The House of Favourite Newspapers

Wasauz Waingilia Dili la Yanga Kwa Tshabalala

0

HERRY Mzozo ambaye ni meneja wa beki wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema kuwa mchezaji huyo anawindwa vikali na klabu za kutoka nchini Afrika Kusini ‘Sauz’. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, beki huyo amefanikiwa kucheza michezo yote akianza kikosi cha kwanza.

 

Iliripotiwa kuwa, anatakiwa na Yanga.Akizungumza na Championi Jumamosi, Mzozo alisema nyota huyo mkataba wake unakaribia kuisha.

 

“Tshabalala bado hajasaini mkataba na Simba, mkataba wake wa awali umesalia miezi miwili ili umalizike na kuna ofa kutoka katika timu za Afrika Kusini ambazo zimeonyesha nia kuwa zinamuhitaji, kuhusu Yanga bado sijapata ofa rasmi, nasikia tu tetesi kuwa wanamhitaji.

 

Lakini Simba bado wana nafasi kubwa ya kumuongezea mkataba kwa kuwa bado ni mali yao ila kama hizo timu kutoka Afrika Kusini zitafika makubaliano mazuri basi sisi hatutakuwa na shida, tutafanya biashara,” alisema meneja huyo.Hivi karibuni kuhusu sakata hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Barbara Gonzalez, alisema:

 

“Tunajua wazi kuwa beki na nahodha wetu Tshabalala mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari zipo timu ambazo zinavutiwa kumsajili lakini niweke wazi kuwa huyo bado ni mchezaji wetu kwa kuwa ana mkataba na Simba, lakini uongozi una matarajio makubwa ya kumpa mkataba mpya ili aendelee kuitumikia klabu yetu.

MARCO MZUMBE,Dar es Salaam

Leave A Reply