The House of Favourite Newspapers

Washambuliaji Wanne Yanga = Meddie Kagere

0

MEDDIE Kagere ambaye ni mshambuliaji wa Simba, ameipoteza safu ya ushambuliaji ya Yanga katika upande wa kufunga mabao. Kagere mwenye mabao 19 msimu huu katika Ligi Kuu Bara, amewazidi bao moja washambuliaji wanne wa Yanga, David Molinga, Ditram Nchimbi, Tariq Seif na Yikpe Gnamien.

 

Wakati Kagere akifi kisha mabao 19, Molinga, Nchimbi, Tariq na Yikpe kwa pamoja wana mabao 18.

Kumbuka hao ndiyo washambuliaji halisi wa timu hizo mbili. Simba ukimuongeza na John Bocco mwenye mabao manne, jumla wanakuwa na mabao 23 ambayo pia kuja kufi kiwa na Yanga wanatakiwa wafanye kazi ya ziada. Katika ligi kuu msimu huu, Molinga ana mabao nane, Nchimbi (6), Tariq (3) na Yikpe (1).

 

Ikumbukwe kuwa, katika mabao sita ambayo Nchimbi anayo kwa sasa, manne aliyafunga akiwa Polisi Tanzania kabla ya kutua Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu. Akiwa Yanga amefunga mawili.

STORI LUNYAMADZO MLYUKA

BREAKING: CORONA, MAGUFULI – “WAGONJWA WAONGEZEKA HADI 12, HAKUNA KIFO CHOCHOTE”

Leave A Reply