The House of Favourite Newspapers

Washia Waadhimisha Kifo Cha Mjukuu Wa Mtume

 washia-1 Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheri ya Tanzania Sheikh, Hemed Jalala akiongea na wanahabari.

washia-2 washia-4 washia-5Baadhi ya waumini wa Dhehebu la Shia wakiendelea na maandamano.

Waumini wa dhehebu la Shia la Msikiti wa Kigogo Post jiji ni Dar, leo wamefanya maandamano ya amani kwa ajili ya kuadhimisha kifo cha mjukuu wa Mtume Mohammad (S.A.W.W ) Imma Hussein (A.s) ambaye aliuwawa kikatili na miili yao kukatwakatwa katika Jangwa la  Karbala nchini Iraq.

Maandamano hayo yamefanyika kuanzia maeneo ya Boma mpaka kwenye makao makuu ya Msikiti Shia uliopo  Kigogo Post, yakihusisha waumini na wasiyo waumini wa dhehebu la Shia.

Akizungumza na wanahabari Kiongozi Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh, Hemed Jalala amesema kuwa Mjukuu wa mtume alipenda amani hivyo wanadamu tunapaswa kuiga mfano wake kwa kukemea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ujambazi, ubakaji, ugaidi, dhuluma, unyanyasaji, ukandamizaji na maovu mengine kama hayo ili kuifanya dunia na wanadamu kuwa kitu kimoja.

Comments are closed.