The House of Favourite Newspapers

Washindi 15 wapatikana promosheni ya Tia kitu pata vituz na DStv!  

Mkuu wa Kitengo cha Thamani kwa wateja MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo akizungumza na waandishi wakati wa droo ya kupata washindi wa awamu ya 3 , kulia ni Afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Humudi Semvua  na kushoto ni Afisa Uhusiano Grace Mgaya.
Mkuu wa Kitengo cha Thamani  kwa wateja MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo  (Katikati) Akizungumza kwa simu na moja ya washindi wa promosheni hiyo. 

 

Kampuni ya MultiChoice nchini kupitia king’amuzi chake cha DStv imechezesha droo yake ya tatu ya promosheni ya “Tia kitu, pata vituz” mapema leo katika makao makuu ya ofisi zake zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuwatangaza washindi hao 15 wa awamu ya tatu, Mkuu wa kitengo cha Thamani kwa wateja MultiChoice Tanzania bi. Hilda Nakajumo alieleza kuwa, “Leo tumefanikiwa kupata washindi 15  washindi waliopatikana kutoka vifurushi vyote vya DStv kama Bomba, Family, Compact, Compact plus pamoja na  Premium.

 

 

Washindi hawa wanafanya jumla ya washindi wetu kufikia 45 tangu promosheni hii ilipoanza  kutokea katika mikoa tofauti hapa nchini kama vile Mwanza, Kagera, Iringa pamoja na Dar es Salaam. Hii inaonyesha wazi kuwa king’amuzi cha DStv kinaendelea kutoa huduma nzuri na gharama nafuu”,alisema Nakajumo.

Aidha amesema kuwa washindi hao wamezawadia malipo ya miezi miwili ya vifurushi vile vile walivyolipia ili kuendelea kufaidika na burudani kedekede kupitia king’amuzi pendwa cha DStv.

 

 

Naye mshindi wa kifurushi cha Compact mkazi wa jijini mwanza, Musa Juma  miaka 24 amewapongeza na kuwashukuru DStv kwa promosheni hiyo ya tia kitu pata vituz . “Sikutegemea kama ningeweza kushinda katika droo hii ya tatu mara nyingi nasikia tu wenzangu wakishinda nikajaribu bahati yangu kwa kufanya malipo kwa wakati na hatimae leo nimeibuka mshindi” alisema Juma.

 

Pia amewapa ujasiri wateja wengine wa DStv kulipa kwa wakati ili kujipatia nafasi hiyo ya kuingia kwenye droo hiyo ya kushinda miezi miwili bila malipo.

Comments are closed.