The House of Favourite Newspapers

Washindi Wa Magifti Dabodabo Ya Tigo Walivyoenda Zanzibar Kuinjoi Siku 4 Na Wapendwa Wao

0
Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta akizungumza kwenye hafla ya kuwaaga washindi hao.

Dar es Salaam, 10 Desemba 2023: Washindi wa Kampeni ya Magifti Dabodabo inayoendeshwa na Kampuni ya Mtandao wa simu za mkononi ya Tigo jana wameenda Kisiwani Zanzibar kuinjoi maisha ambapo watafikia hoteli kwenye hoteli ya kisasa ambapo watakaa siku nne na kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii.

Kama ilivyo kampeni hiyo ya Magifti Dabodabo ukishinda kitu unamchagua wa kushinda nae hivyo washindi hao nao waliambatana na wapendwa wao ambapo wapo walienda na wake zao, marafiki, familia, ndugu na wapendwa ujumla.

Akizungumza kwenye hafla ya kuwasindikiza washindi hao iliyofanyika Bandarini Dar, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;

Shangwe zikiendelea eneo la Bandarini kwenye hafla ya kuwasindikiza washindi hao.

“Tumekuja hapa kuwasindikiza washindi wetu wanaoenda Zanzibar kwenye kampeni inayoitwa Magifti Dabodabo, washindi hawa wamepata hii nafasi kwa kutumia huduma za mbalimbali za Tigo kama vile kununua vifurushi kwa njia yeyote ile, kufanya miamala ya Tigo Pesa na huduma nyinginezo.

Washindi hawa wakiwa Zanzibar watafikia kwenye hoteli ya kisasa na watainjoi maisha kwa siku nne na wanatarajiwa kurudi siku ya siku ya Jumatano.

Baadhi ya magari ya kisasa yanayosubiri washindi.

Pamoja na kuinjoi mambo mbalimbali wataenda kutembelea vivutio vya mji wa Zanzibar, uzuri wa Tigo ni kwamba ukishinda chochote tunamjiftisha na yule unayempenda kwahiyo hawa washindi wetu nao wamekuja na wapendwa wao kuwasindikiza kwenye safari hii ambayo imeshalipiwa kila kitu.

Mshindi wa Magifti Dabodabo, Aisha Kajuri akizungumza furaha waliyonayo kwa niaba ya wenzake muda mfupi kabla ya kupanda boti kuelekea Zanzibar.

Hivyo tunawasihi wananchi kutumia mtandao wa Tigo kwani zawadi bado zipo nyingi, kuna zawadi za pesa, vifaa vya nyumbani vya umeme na kuna zawadi kubwa kabisa ya gari kwahiyo inachotakiwa ndugu mwananchi tumia huduma za Tigo ili huweze kuibuka mshindi kwani kampeni hii bado inaendelea mpaka mwakani.

Mmoja wa washindi hao aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Kajuri amesema safari imekuwa ya furaha sana kwao kwani wataenda kutembelea vivutio vilivyopo kisiwani humo na kuinjoi mambo mengi wakiwa na wapendwa wao.

Alimalizia na kuishukuru Tigo kwa kuwapa fursa hiyo adhimu na kuwasihi wananchi wengine kutumia huduma za Tigo kufanya miamala ya Tigo Pesa kwa kulipa bili, kununua muda wa maongezi kwa njia yeyote na mengineyo ili nao waweze kuibuka na ushindi.

Leave A Reply