WASHINDI wa droo ya tano na sita wa Shindano la Tusua Maisha na Global inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers chini ya udhamini wa Sokabet, wamekabidhiwa zawadi zao leo, Agosti 10, 2018 katika ofisi za Global Publishers, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Waliokabidhiwa zawadi zao ni Emanuel Tenga, mkazi wa Moshi aliyewakilishwa na kaka yake, Elinami Mmari na Erasto Luponela, mkazi wa Makambako waliojinyakulia pikipiki, Catherine Tuli, mkazi wa Mbagala na Augustine Haule, mkazi wa Kinyerezi waliojishindia dinner set.
“Tumekabidhi zawadi leo, kwa wale walioshindwa kufika, tumezituma zawadi kwa mawakala wetu wa mikoani ambao watawapigia simu na kuwapa maelezo ya namna ya kubadhiwa zawadi hizo,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Kampuni ya Global Publishers.
Baada ya makabidhiano hayo, washindi wote walipata fursa ya kueleza ya moyoni, na jinsi walivyopokea zawadi zao kwa furaha.
Wakati washindi hao wakikabidhiwa zawadi zao leo, tayari washindi wengine wa droo ya saba wameshapatikana ambapo msomaji Said Katambo wa Nachingwea, Lindi ameibuka mshindi wa pikipiki mpya.
Mbali na Said, wengine waliong’ara katika droo ya saba ni Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam aliyejishindia dinner set, Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia head phones za kisasa za Beats by Dre na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu aliyejishindia jezi mpya.
Namna ya kushiriki ni rahisi sana cha kufanya nunua gazeti lako lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Amani, Ijumaa, Risasi, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra, kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya jinsi ya kushiriki.
Itume namba maalum inayoonekana juu ya kuponi hiyo kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kiopande cha kuponi yako au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukua zawadi.
Comments are closed.