Washindi wa Magift ya Kugift Droo ya 6, Leo Vicheko Kama Vyote

Dar es Salaam, 20 Desemba 2024: Watumiaji wa mtandao wa simu wa Yas kupitia Kampeni yake inayoendelea ya Magift ya Kugift leo imeendelea ambapo washindi wa droo ya sita wamepatokanan na kukabidhiwa zawadi zao walizojishindia.
Washindi hao walikabidhiwa hundi ya fedha walizojishindia na msemaji wa kampeni hiyo, Haji Manara maarufu kama Bugati aliyekuwa sambamba na Meneja wa Wateja Maalum wa Mixx By Yas, Mary Rutta.
Baada ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao Bugati aliwataka watumiaji wengine wa simu kutumia mtandao wa Yas kwa ajili ya huduma mbalimbali ikiwemo kununua salio kupitia Mixx By Yas, kutuma pesa mitandao mingine, kufanya miamala mbalimbali kama vile kuweka na kutoa pesa, kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia Mixx By Yas (zamani Tigo Pesa). Bugati aliendelea kusema kuwa kwa kufanya hivyo unakuwa umeingia kwenye droo ijayo hivyo kuweza kuondoka na zawadi mbalimbali kama vile simu janja, pesa taslimu shilingi milioni moja au kumi na unaweza kufurahia vyema kipindi hiki cha sikuu za Krismas na Mwaka mpya. Alimaliza kusema Bugati.