testiingg
The House of Favourite Newspapers

Washindi wa Serengeti Maokoto Ndani ya Kizibo Wakabidhiwa Zawadi Zao

0

Washindi wa Kampeni ya Serengeti, Maokoto Ndani ya Kizibo wanazidi kujizolea zawadi mbalimbali katika droo zinazoendelea kuchezeshwa.

Balozi wa kampeni ya Maokoto ndani ya Kizibo, Billnass (kulia) akimkabidhi mfano wa Hundi mmoja wa washindi wa kampeni hiyo, Juliana Joseph( kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika katika Baa ya Dagaa Dagaa, jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita.
Mwakilishi wa Serengeti Breweries Manispaa ya Iringa Doreen Mchau kushoto pichani akimkabidhi mfano wa Hundi ya Laki tano Agritha Mbilinyi Mshindi wa Drow ya  Maokoto Serengeti Ndani ya Kizibo wakati wa hafla fupi iliyo fanyika katika ukumbi wa Royal Tour Pub mtaa wa Samora Manispaa ya Iringa jana.
Msimamizi wa Promosheni ya Maokoto Ndani ya Kizibo  wa Kampuni ya Serengeti Breweries Kanda ya Ziwa, Raphael Mkama (kushoto) na Afisa Masoko wa kampuni hiyo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Majura Chigilo, wakionesha mfano wa hundi ya Sh laki 5 ambayo ni zawadi ya mshindi wa Maokoto, Elias James mkazi wa Sengerema aliyeshinda kiasi hicho, lakini hakuwepo kwenye hafla ya makabidhiano kutokana na dharura ya kifamilia, hafla ilifanyika katika baa ya California A.
Mwwakilishi wa SBL, Cherestisto Kiwelo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi laki tano Johari Shabari kutoka Kisasa Dodoma aliyejishindia maokoto ya SBL kutoka mkoa wa Dodoma. Johari alizawadiwa shilingi laki 5.
Doreen Tagalile, Afisa Mauzo Kanda ya Dar es Salaam Kusini (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi laki tano za Kitanzania mshindi wa Maokoto Ndani ya Kizibo, Tumaini Ndumbaro, Svoy Lounge, Buza jijini Dar es Salaam wikiendi hii.
Leave A Reply