The House of Favourite Newspapers

WASHINDI WA TIGOPESA WAKALA PROMOSHENI WAKABIDHIWA ZAWADI

 

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Angelica Pesha akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi watatu wa promosheni ya Tigopesa Wakala, Dar es Salaam . Kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa (kushoto).
Kampuni ya simu ya Tigo leo imetoa zawadi kwa washindi watatu wa promosheni ya tatu ya mawakala wa Tigo Pesa ikiwa ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa mawakala wao nchi nzima. Promosheni hiyo ijulikanayo kama ‘Tigo Pesa Wakala promosheni’ ilianza mwezi Septemba 2019 ambapo washindi 12 wametoka katika kanda nne za Tigo(kanda ya Ziwa, Pwani, Nyanda za juu kusini na Kaskazini).
Promosheni hii ni kwaajili ya kutoa shukrani kwa mawakala wa Tigo Pesa zaidi ya 100,000 nchi nzima.Promosheni hiyo ambayo inafayika kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja inamzawadia wakala ambae amefanya miamala mingi katika kanda yake kwa mda wa mwezi mmoja.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Kaimu Mkuu wa kitengo cha Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema “Kwanza niwashukuru na kuwapongeza sana mawakala wetu wote kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhudumia wateja nchi nzima na pili niwapongeze mawakala hawa watatu kwa kuibuka na ushindi kwa kuwapiku maelfu ya mawakala kweye mikoa yao.”

Angelica Pesha (kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3/- kwa mshindi wa tatu wa promosheni ya ‘Tigopesa Wakala’, Vicky Ibrahim katika hafla hiyo
 Pesha alisema huduma ya Tigo pesa imekuwa zaidi ya mfumo wa kutuma na kupokea pesa bali ni sehemu ya shughuli zilizoanzishwa na Tigo Pesa katika kuhakikisha inachangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi hapa nchini hasa kwa njia ya kuwawezesha mawakala wa Tigo Pesa.
“Kama kampuni ya kidigitali tunahakikisha tunakuja na mikakati mbalimbali ambayo itawafanya mawakala nchi nzima kunufaika na huduma hii.Tuna furaha kuchangia agenda ya ujumuishwaji wa watu kiuchumi kupitia huduma ya Tigo Pesa kwa kurahisisha huduma za kifedha jambo linalochochea ukuaji wa uchumi kwa mawakala, jamii pamoja na nchi kwa ujumla,” alisema Pesha.
Baaa ya kutangazwa,washindi walijawa na nyuso za furaha akiwamo Suleiman Hussein kutoka Zanzibar aliyeshinda Sh5 Milioni, Vicky Ibrahim wa Temeke aliyeibuka na Sh3 milioni na Anna Mosha kutoka Ilala aliyejishindia Sh2 milioni.  

Washindi wa promosheni ya Tigopesa Wakala wakiwa kwenye picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tigopesa wa Kampuni ya Tigo, Angelica Pesha (kulia) na Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani wa Tigo, Joseph Mutalemwa (kushoto)
Tigo Pesa inashika nafasi ya pili hapa nchini kama mtoa huduma za kifedha mkubwa kwa njia ya simu.  Tigo Pesa pia imefungua milango ya ugunduzi wa kidijitali Afrika Mashariki ikiwa ni kampuni ya kwanza kuanzisha huduma ya kutuma fedha kwa njia ya simu kwa nchi nyingine, kutuma pesa kwenda mitandao mingine na kuingia kwenye pochi moja, huduma ya jihudumie mwenyewe pamoja na App ya kisasa ya Tigo Pesa inayorahisha sana kufanya miamala.
Ikiwa imezinduliwa mwaka 2010, Tigo Pesa imepiga hatua kutoka kuwa huduma za kutuma na kupokea pesa hadi kutoa huduma zote za kifedha ikiwamo malipo ya kibishara suala linalochangia ustawi wa watu kiuchumi nchini. Tigo Pesa ni huduma ya kifedha inayokua kwa kasi zaidi nchini ikiwa na wateja waliosajiliwa zaidi ya 7 milioni na wafanyabiashara 50,000 pamoja na mawakala zaidi ya 100,000 nchi nzima.

Comments are closed.