The House of Favourite Newspapers

WASHINDI WA WEKA AMANA NA BENKI YA CBA WAPATIKANA

0
Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini ,Abdallah Hamedi(kushoto)akiwaonyesha Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya CBA,Mussa Kitambi (katikati) na mkuu wa taasisi za benki hiyo,Judith Mkama namba ya mshindi wa droo ya Nne ya promosheni ya akiba ya ‘Weka amana ushinde’inayoendeshwa na benki hiyo wakati wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha Sandeep Kumali alijishindia kitita cha shilingi milioni 1/ na Roman Attorneys ilijishindia kitita cha shilingi milioni 2/- .Zaidi ya milioni 20 zinashindaniwa na wateja wa benki hiyo.
Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya CBA, Mussa Kitambi(Katikati) akimpigia simu mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam, Roman Attorneys aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 2/- wakati wa droo ya Nne ya promosheni ya akiba ya‘Weka amana ushinde’ iliyofanyika jijini Dar es Salaam,Kuna zaidi ya shilingi milioni 20 zinashindaniwa na wateja wa benki hiyo,Kushoto ni Msamimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini ,Abdallah Hamedi na Mkuu wa taasisi za benki hiyo,Judith Mkama.

 

BENKI ya CBA, leo iliendesha droo yake ya Nne katika kampeni ya kuhamasisha umma kujiwekea akiba inayojulikana kama ‘weka amana ushinde’ ambapo washindi wawili walipatikana na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu

 

Sandeep Kumali kutoka Arusha aliibuka mshindi kwa upande wa wateja binafsi na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 1/=, huku Kampuni ya Roman Attorneys ya jijini Dar es Salaam wakiibuka washindi katika upande wa taasisi na kujinyakulia shilingi milioni 2.

 

Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetengwa kwa ajili ya kutolewa kama zawadi katika kampeni hiyo ambayo itakayodumu kwa kipindi cha miezi mitatu.

 

Akizungumza muda mfupi baada ya kuchezeshwa kwa droo hiyo ambayo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki ya CBA, Mussa Kitambi alisema lengo la promosheni hiyo ni kuhamasisha umma kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.

 

”Kampeni hii inalenga kuwahamasisha wateja wetu waliopo na watarajiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba. Kuweka akiba ni muhimu kwa kuwa kunawezesha kufanya uwekezaji pamoja na kupambana na matukio yasiyotarajiwa ambayo yanahitaji fedha,” alisema Kitambi

 

Alisema kujiwekea akiba ni muhimu haswa katika kipindi hiki kinachoelekea mwisho wa mwaka ambapo huwa na mahitaji makubwa ya kifedha kwa ajili ya shughuli kama kulipa ada za shuke, kodi za nyuma, likizo pamoja na shughuli nyingine

 

Kwa mujibu wa Kitambi, benki ya CBA imerahisisha namna ya wateja wake kujiwekea akiba ambapo wanaweza kutumia simu zao za kupitia huduma ya M-PAWA, kwa kutumia njia ya mtandao pamoja na kutembelea matawi yake yaliyopo sehemu mbali mbali.

 

Benki ya CBA kwa sasa ina matawi 11, matano yakiwepo jijini Dar es Salaam huku matano yakiwepo Arusha, Mwanza, Mbeya, Mtwara, Moshi, na Tunduma.

 

NA DENIS MTIMA

Leave A Reply