Washukiwa wa bomu bandia ndege ya Air France wakamatwa Ufaransa

Air france (2)Abiria wa ndege hiyo wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenya baada ya kuokolewa.

MAOFISA wa Polisi nchini Ufaransa wamewatia mbaroni abiria wawili wa ndege hiyo ambao ni mke na mme liokuwa abiria katika ndege ya Air France Boeing 777 nambari AF463 iliyolazimika kutua kwa dharura nchini Kenya hapo jana kufuatia tishio la bomu.

Air france (1)Duru zinasema kuwa wawili hao ambao majina yao bado hayawekwa hadharani walikamatwa punde baada ya kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Charles de Gaulle nchini Ufaransa.

An Air France jet liner which made an emergency landing is seen at Moi International Airport in Mombas, Kenya Sunday, Dec. 20, 2015. The Boeing 777 Air France flight 463 from Mauritius to Paris was forced to land in the Kenyan coastal city of Mombasa after a device suspected to be a bomb was found in the lavatory, a Kenyan police official said Sunday. (AP Photo/Edwin Kana)Ndege ya shirika la Air France.

Waliokamatwa ni ofisa mmoja mstaafu wa polisi ambaye ni mshukiwa mkuu huku mkewe akishikilwa ili kutoa shahidi wa tukio hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Air France alifutilia mbali tahadhari ya bomu iliyosababisha ndege hiyo ya kutua kwa dharura Kenya na kusema kuwa lilikuwa bomu bandia.

Air france (3)Abiria baada ya kuokolewa.

Frederic Gagey aliwaambia waandishi wa habari mjini Paris, Ufaransa kuwa kifaa kilichodhaniwa kuwa kilipuzi kilikuwa ni mbao na kisanduku cha karatasi tu wala hakikuwa na uwezo wowote wa kuhatarisha usalama wa ndege hiyo.

AirFrancAbiria baada ya ndege hiyo kutua kwa dharura Kenya.

Inasemekana kuwa abiria mmoja alikipata kifaa hicho chooni na akamfahamisha mhudumu mmoja wa ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 459 na wahudumu 14.

Air_France_confirmedBomu bandia lililokutwa kwenye ndege hiyo

Mhudumu huyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho na shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.

Ndege hiyo ilitua saa sita usiku wa kuamkia Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka jeshi la wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua kifurushi kilicholeta taharuki.

Sasa kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kimeanzisha uchunguzi wa kina kubaini kilichosababisha tishio hilo.

PICHA NA DAILY MAIL


Loading...

Toa comment