The House of Favourite Newspapers

Wasichana Watano wanamuziki wenye mkwanja Uingereza

0

Na Mwandishi Wetu

WAKATI mamia ya wasanii wa Kitanzania wamekuwa wakipigana ili kupata majina makubwa ili kuwemo miongoni mwa mastaa, wenzao akili zao zimeelemea zaidi katika kutengeneza fedha zinazoishi.

Wakati mkali wa Hip Hop Sean John maarufu kama P Diddy akiongoza miongoni mwa wanamuziki walioingiza fedha katika muziki kwa jumla mwaka jana kwa mujibu wa Jarida la Forbes, nchini Uingereza, wafuatao ndiyo wasichana wenye umri mdogo wanaomiliki fedha nyingi zaidi.

Adele

NI msanii ambaye jina lake halisi ni Adele Laurie Blue Adkins, aliyezaliwa Mei 5, 1988 huko Tottenham, jijini London.

Akiwa na mpenzi wake Simon Konecki tangu mwaka 2011 na mtoto mmoja, msichana huyo mwenye umri wa miaka 27 ana mkwanja unaofikia pauni milioni 50, karibu shilingi bilioni 125.

Ana tuzo kadhaa zikiwemo sita za Grammy Awards alizopata mwaka 2012 zikijumuisha albamu bora ya mwaka. Ni staa anayesumbua katika muziki wa Ulaya na Marekani akiwa ameuza jumla ya nakala milioni 30 za albamu yake ya 21 dunia nzima

Cheryl Cole

JINA alilopewa baada ya kuzaliwa ni Cheryl Ann Tweedy, lakini alikuja kufahamika zaidi kama Cheryl Cole baada ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na kuolewa na beki za zamani wa England, Ashley Cole kabla ya kutengana Septemba 2010.

Akiwa amezaliwa Juni 30, 1983 mwimbaji huyo wa Kundi la Girls Aloud ana ukwasi wa kiasi cha pauni milioni 14, zaidi ya pesa ya madafu kama shilingi bilioni 35 za Kibongo.

Ana tuzo nyingi alizopata akiwa peke yake na kundi kabla halijavunjika mwaka 2013, lakini anasifika kwa singo zake tatu zilizompa mafanikio makubwa, ikiwemo Fight For This Love, iliyowahi kutingisha katika chati za Uingereza na iliyouzwa zaidi mwaka 2010.

Leona Lewis

Jina lake ni Leona Louise Lewis ambaye alizaliwa Aprili 3, mwaka 1985 katika kitongoji cha Islington, jijini London ambaye licha ya kuimba, lakini pia ni mwandishi wa nyimbo na mwanaharakati wa kutetea haki za wanyama.

Akiwa ameibuliwa na shindano la kila mwaka la X Factor mwaka 2006, akishinda mkataba wa kurekodi wa pauni milioni moja na lebo ya Syco Music ya Simon Cowell, Leona ana mtonyo unaokadiriwa kuwa pauni milioni 12, zikiwa ni zaidi ya pesa za madafu shilingi bilioni 30.

Ni mmoja kati ya wanamuziki wenye mafanikio makubwa katika Uingereza na moja ya rekodi alizojiwekea ni pamoja na singo yake ya A Moment Like This, ilipochukuliwa katika mtandao mara 50,000 ndani ya nusu saa wakati ilipotoka mwaka 2006.

Katie Melua

Katie Melua ambaye jina lake la kuzaliwa ni Ketevan Melua, alizaliwa Septemba 16, 1984 huko Kutaisi, Urusi. Akiwa ameingia Uingereza akiwa na umri wa miaka 14, Melua alijulikana katika ulimwengu wa muziki mwaka 2003 na miaka mitatu baadaye, akawa msanii wa kike anayeuza zaidi katika nchi hiyo ya kifalme na barani Ulaya kwa jumla.

Kama Leona, Katie naye na ‘mpunga’ wa zaidi ya bilioni 30, sawa na pauni milioni 12.  Kulingana na Jarida la Sunday Times Rich List 2008, Melua alikuwa na utajiri wa pauni milioni 18, akiwa wa saba kati ya wasanii matajiri chini ya umri wa miaka 30, lakini anadaiwa kunusurika kufilisika baada ya mdororo wa uchumi duniani mwaka 2009.

Florence Welch

Akiwa na umri wa miaka 29, akizaliwa Agosti 28, 1986, jina lake halisi ni          Florence Leontine Mary Welch kutoka Camberwell, England.

kama albamu bora mwaka 2010.

Msichana huyu ana mkwanja unaotajwa kuwa ni pauni milioni 9, zinazopita kidogo kiasi cha shilingi bilioni 22.5 za Kibongo.

Leave A Reply