WASOMAJI: BETIKA LINATUPA FAIDA MARA MBILI
GAZETI la Betika likiwa na wiki ya 24 mtaani, limeendelea kuwa kipenzi cha wasomaji wengi huku wakisema linawapa faida mara mbili.
Betika ambalo linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na linaingia mtaani kila Jumatano.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi tofauti duniani.
Kila linapoingia mtaani, maofisa masoko wa Global Publishers hutembelea mitaa mbalimbali na leo walikuwa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni na Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Wasomaji kadhaa waliofanya mahojiano juu ya gazeti hilo, wameonekana kulikubali huku wakipongeza namna ambavyo lilivyokuja tofauti.
“Kuhusu Betika, linawasaidia wengi, hata mimi linanisaidia kwani huwa najihusisha na masuala ya kubeti na humu ndani kuna mambo yote kuhusiana na ishu hizo.
“Lakini pia kuna haya matangazo yaliyopo, unapokuwa na Betika, unafaidika nalo kwa mambo mengi, kwanza kupata mwanga wa kubeti, lakini kupitia matangazo, mtu unafahamu mambo mengine nje ya soka,” alisema Juma Issa mkazi wa Kinondoni.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema heshima ya Betika imeendelea kukua kila siku na sasa wanajivunia kuwa na idadi kubwa ya makampuni yanayotangaza biashara zao kupitia gazeti hilo hasa kwa kuwa bei yao ni nafuu na imewavutia wengi, huku akiongeza kuwa bado wanawakaribisha watu binafsi na makampuni kuleta matangazo yao.
“Hili ni gazeti la bure, linawahusu watu wazima kuanzia umri wa miaka 18, linatolewa bure kabisa kwa wauza magazeti wote nchini.
“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0712595636 au barua pepe [email protected], bei zetu ni nafuu, muhusika anaweza kufika Sinza Mori, Dar, kwenye jengo letu la Global Group.
“Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao yetu ya kijamii katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online,” alisema.
Comments are closed.