The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Kutusua Maisha na Global Kuanzia Kesho (Picha + Video)

Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akiongea na wanahabari wakati wa kuzindua promosheni ya ‘Tusua Maisha na Global’ leo katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori, Dar es Salaam.

 

KUANZIA kesho (Ijumaa) Kampuni ya Global Publishers itaanza kuendesha shindano maalum lililopewa jina la ‘Tusua Maisha na Global’ kwa ajili ya wasomaji wake ambao watajishindia pikipiki ambapo kila wiki itatoka moja.

 

Wasomaji wa Magazeti ya Michezo ya Championi, yanayotoka siku nne kwa wiki, yani Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi na Spoti Xtra linalotoka kila Jumapili na Magazeti Pendwa ya Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani na Uwazi, watafaidika.

Shindano hilo litafanyika kwa muda wa miezi mitatu kuanzisha kesho.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 

Pikipiki 12 zimetengwa kwa ajili ya wasomaji hao ambapo kila wiki itatoka moja pamoja na zawadi zingine za  simu, fulana, ada ya shule na vyombo vya ndani.

 

Namna ya kucheza shindano hilo:

Mshiriki nenda sehemu ya kutuma ujumbe (SMS), kwenye simu yako, andika namba  zilizopo kwenye kuponi ukurasa wa pili wa gazeti husika, kisha utatuma namba hizo kwenda namba 0719 386 533. (Hakikisha una salio au bando la kutuma meseji kwa kiwango cha kawaida tu).

Kisha jaza taarifa zako binafsi kwenye kuponi hiyo na tunza nakala ya gazeti lako kwani litahitajika wakati wa kuchukua zawadi yako.

Wafanyakazi wa Global Publisher baada ya uzinduzi huo.

 

Kwa kutuma ujumbe, moja kwa moja unakuwa umengia kwenye kinyang’anyiro cha kujishindia  zawadi ya pikipiki na zawadi nyingine zitakazotolewa kila wiki.

 

Namba yako itaingizwa kwenye droo itakayochezeshwa kila Jumamosi na kuonyeshwa moja kwa moja mtandaoni na Global TV Online. Utapigiwa simu iwapo utafanikiwa kujishindia zawadi yoyote kwa wiki husika.

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers, Amrani Kaima (kulia) akiwa na wafanyakazi wenzake.

 

Kwenye gazeti kutakuwa na kuponi yenye taarifa zifuatazo; Jina kamili, namba ya simu, umri na mahali unapoishi.

Hata hivyo, msomaji anatakiwa kufahamu kuwa ili ithibitike kuwa yeye ndiye mshindi anatakiwa kutumia namba ya simu  iliyosajiliwa kwa jina lake, anatakiwa kuwa na kuponi iliyomfanya awe mshindi wakati wa kwenda kuchukua zawadi yake.

Ni furaha tupu miongoni mwa wafanyakazi wa Global Publishers wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.

Kama jina lililosajiliwa kwenye simu litakuwa tofauti na jina la mtumiaji, basi hatapewa zawadi husika.

Pia Global Publishers inapenda kuwataarifu wasomaji wake kuwa, gazeti moja litatumika kwa SMS moja tu na siyo vinginevyo.

Comments are closed.