Wasomaji Mbagala Watamba Kunyakua Ndinga ya Championi, Spoti Xtra

Wasomaji wa magazeti ya bora ya michezo yanayoongoza kwa habari za uhakika zilizofanyiwa uchunguzi wa kina Championi na Spoti Xtra, maeneo ya Mbagala jijini Dar, jana Alhamisi walizidi kuchangamkia shindano la kubwa la Baba lao ambapo mshindi anatarajiwa kuondoka na gari mpya aina ya Toyota FunCargo.

Kitengo cha Masoko na Usambazaji cha magazeti hayo, jana kilingia maeneo mbalimbali ya mbagala na kuzungumza na wasomaji hao na kuwahamasisha wasomaji magazeti ya michezo kujipatia magazeti hayo na kushiriki Bahati Nasibu hiyo.
Wasomaji walionekana kuhamasika na kuyachangamkia magazeti hayo na kujaza kuponi inayoelekeza jinsi ya kushiriki shindano hilo huku wakijitapa kuinyakua ndinga hiyo.

Akizungumza na wasomaji hao, Mkuu wa Idara ya Masoko na Usambazaji, Anthony Adam aliwaambia wasomaji hao gari hiyo hiyo inatarajiwa kukabidhiwa kwa mshindi muda si mrefu kuanzia sasa.
Anthony amesema pamoja na gari hiyo washindi wengine watajinyakulia zawadi mbalimbali kama vile simu za kisasa za mkononi (smart phone) pesa taslimu na zawadi nyinginezo.

Ambapo pia aliwasisitiza wasomaji hao kuzidi kujisomea magazeti hayo na kuchana kuponi iliyopo ukurasa wa pili kwenye magazeti hayo na kumkabidhi muuza magazeti yeyote aliye karibu nao kwa ajili ya kuweza kujishindia gari zawadi hizo.
-Picha mbalimbali za wakazi wa Mbagala walivyotembelewa na kikosi cha mauzo na usambazaji
HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS/GPL

