The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Tabata-Chawote Wamelikubali Kinoma ‘Betika’

MAPEMA leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishers imetembelea maeneo ya Tabata-Chawote, Makamba FC, TOT, Ally Hamza, Twiga-Tabata na maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulitangaza zaidi gazeti la Betika.

Wakilielezea gazeti la Betika, wasomaji hao wamesema kila siku ya Jumatano ambapo Betika hutoka, huwa hawalikosi kutokana na umuhimu wa gazeti hilo kwao kuwawezesha kupata nondo za maana zinazowasaidia KUBETI na kushinda mkwanja mara kwa mara.

Betika ambalo hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano ya wiki.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti za ndani ya Tanzania na Ulaya pamoja na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kuwa gumzo kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Heshima ya Betika imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia gazeti hilo  kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.