Msomaji wa gazeti la Amani, Crispin Rojas (kushoto) akijaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Katikati ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Mkanda (kulia) akimsaidia kujaza kuponi msomaji wa Amani aitwaye, Abdallah Sufian.
Sufiani (kulia) akipewa maelekezo ya kujaza kuponi kwenye gazeti la Amani.
Msumi Hamad akielekezwa namna ya kujaza kuponi yake na Mkanda.
Mdau wa gazeti la Amani aliyejitambulisha kwa jina moja la Imma (kulia) akipata maelekezo ya kujaza kuponi yake kutoka kwa Mkanda.
WASOMAJI wa gazeti la Amani wa eneo la Biafra- Kinondoni Dar, leo walichangamka na kulinunua kwa kujaza kuponi kwa wingi kuelekea droo kubwa ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba iliyobakiza siku 21 ambapo mshindi atakabidhiwa nyumba iliyopo eneo la Salasala Kinondoni, Dar.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alifika eneo hilo na kukuta wasomaji wa Amani wakiwa na gazeti hilo na kuwapa maelekezo ya namna ya kushiriki bahati nasibu hiyo.
Mkanda alisema: “ Siku zimebaki 21, wakazi wa Biafra changamkieni fursa hiyo na mshindi wa nyumba anaweza kuwa miongoni mwenu, hivyo nunueni magazeti mengi ya Global na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda.”
NA DENIS MTIMA/GPL