Wasomaji Wachangamkia Droo ya Pili ya Shinda Nyumba
Msomaji wa Gazeti la Championi (wapili kushoto) akielekezwa na Maofisa Usambazaji wa Global, Jordan Ngowi (kushoto) na (wapili kulia), Yohana Mkanda. Aliyeshikilia magazeti ni muuzaji wa magazeti ya Global.
Wasomaji wa Magazeti ya Championi na Ijumaa wa eneo la Kimara Suka wakipatiwa zawadi za kofia mara baada ya kununua magazeti na kukata kuponi.
…. Wakikata kuponi na kuweka kwenye ndoo maalum ili kushiriki droo ya pili ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Ofisa usambazaji wa Global, Jordani Ngowi (mwenye fulana nyeupe) akiwaelekeza wasomaji namna ya kujaza kuponi kwenye gazeti.
…. Yohana Mkanda (kulia) akimvalisha kofia msomaji wa Kimara Suka baada ya kununua gazeti.
Maofisa hao, Ngowi na Mkanda wakimwelekeza msomaji wa Gazeti la Ijumaa namna ya kushiriki Bahati nasibu hiyo eneo la Kimara Mwisho.
Zawadi za kofia zikitolewa kwa wasomaji.
Ngowi (kulia) akimvalisha kofia msomaji.
Mkanda (kulia ) akimwelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi.Wasomaji wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Global (wenye fulana nyeupe).
Wasomaji wakivalishwa kofia baada ya kumaliza zoezi la kuweka kuponi kwenye ndoo maalum eneo la Mbezi Mwisho.
Wasomaji wa Mbezi Mwisho wakiwa wamelizunguka gari la matangazo la Global ili wanunue magazeti.
… wa eneo la Mbezi Mwisho wakichangamkia kununu magazeti.
Wakiweka kuponi zao kwenye ndoo maalum ili kushiriki droo ya pili ya Bahati nasibu itakayochezeshwa mwanzoni mwa mwezi ujao.
WASOMAJI wa magazeti pendwa ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi na Ijumaa Wikienda pamoja na yale ya michezo ya Championi wamezidi kujitokeza kwa wingi katika kuchangamkia fursa ya droo ya pili ya Bahati nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.
Kampuni hiyo leo jijini Dar imetoa zawadi kwa wasomaji wake baada ya kununua magazeti kwa wingi ili kukata kuponi kwa ajili ya kushiriki Bahati nasibu hiyo inayotarajiwa kuchezeshwa mwanzoni mwa mwezi ujao.
Baadhi ya wasomaji waliojinyakulia kofia zilizo na nembo ya Shinda Nyumba ni pamoja na wakazi wa Kimara Suka, Mbezi mwisho na Kinyerezi na kwingineko.
Kupitia Bahati nasibu hiyo msomaji anachotakiwa kufanya ni kununua nakala moja au zaidi ya magazeti na kukata kuponi moja iliyo katika kila gazeti kisha kujaza jina lake kamili na anuani yake na kutuma kwa njia ya Posta, kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga-Mwenge au kuzipeleka kwa mawakala wa kuuza magazeti popote ulipo nchini.
Aidha nyumba inayoshindaniwa imejengwa eneo la Salasala-Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa na samani za ndani na itatolewa mwishoni mwa mchezo huku droo nyingine ndogo zikichezeshwa kila mwezi, ambapo simu mpya za kisasa, runinga na ving’amuzi hutolewa.
Katika shindano hili watu walio chini ya umri wa miaka 18, ndugu wa wafanyakazi wa Global Publishers hawaruhusiwi kushiriki.
Na Denis Mtima/Gpl