The House of Favourite Newspapers

Wasomaji Wa Spoti Xtra Wazawadiwa Vitu Mbalimbali

Msomaji wa Spoti Xtra aliyelinunua huko Mwenge (kulia), Dar es Salaam, akipatiwa zawadi ya sabuni na muuzaji wa magazeti hayo.
Ofisa Masoko wa Spoti Xtra, Jimmy Haroud (kushoto) akiwa na msomaji wa gazeti hilo aliyemzawadia sabuni baada ya kulinunua.
Msomaji wa gazeti la Spoti Xtra akilisoma baada ya kulinunua sehemu za Mabibo, Dar es Salaam.
Msomaji wa Spoti Xtra akilisoma baada ya kulinunua na kupewa zawadi sehemu za Tabata, Dar es Salaam.
Msomaji wa Spoti Xtra wa Temeke, Dar es Salaam, akiwa amejikita katika kulisoma gazeti hilo.
Eneo la Manzese, Dar es Salaam, kamera yetu ilimkuta mwananchi huyu akiwa analisoma Spoti Xtra kwa makini.

Wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra walionunua gazeti hilo kwenye msafara wa promosheni uliokuwa ukipita viunga mbalimbali vya jiji la Dar, leo Jumapili walizawadiwa zawadi mbalimbali zikiwemo sabuni, dawa za meno na nyinginezo.

 

Katika promosheni hiyo wasomaji waliendelea kulisifia gazeti hilo kutokana na ubora, habari zake na makala zilizochambuliwa na waandishi wazoefu.

 

Wasomaji hao walipatiwa nafasi ya kutoa maoni yao ambapo walitoa maoni mbalimbali ambayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

 

Msafara huo ulikatiza katika viunga  vya jiji la Dar ambapo ulianzia Sinza-Mori, na kuelekea Mwenge, Manzese Kwa Mfuga Mbwa, Soko la Ndizi Mabibo, Kigogo-Luhanga, Kigogo Mwembe-Jando, Tabata-Dampo na maeneo mengine ambapo wasomaji walionunua gazeti hilo walipewa zawadi.

(Picha Na Richard Bukos)

Comments are closed.