The House of Favourite Newspapers

Wasomaji wachangamkia droo ya kwanza Shinda Nyumba kesho!

0

????????????????????????????????????

Muuza magazeti wa Kampuni ya Global Publishers (mwenye fulana nyeupe), akimuelekeza msomaji jinsi ya kujaza kuponi na kushiriki bahati nasibu hiyo ambayo kesho itafanyika droo ya kwanza.

????????????????????????????????????

Zoezi la kujaza kuponi ili kushiriki droo ya kwanza ya bahati nasibu kesho likipamba moto.

????????????????????????????????????

Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kushoto) akishudia msomaji wa Gazeti la Championi akijaza kuponi ili kushiriki droo ya kwanza inayotarajia kuchezeshwa kesho.

????????????????????????????????????

Mkazi wa Vingunguti akiweka kuponi yake tayari kwa ajili ya kushiriki droo ya kwanza ya Shinda Nyumba.

????????????????????????????????????

Ofisa Masoko, Yohana Mkanda (kulia) akimwelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi.

????????????????????????????????????

Msomaji wa Gazeti la Risasi Jumatano wa eneo la Buza, Dar akijaza kuponi yake ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

????????????????????????????????????

Mwanadada aitwaye Mariam mkazi wa eneo la Buza, Dar, akijaza kuponi mara baada ya kununua gazeti.

????????????????????????????????????

Kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya eneo la Temeke na Buza, akijaza kuponi kwa ajili ya kushiriki bahati nasibu hiyo.

????????????????????????????????????

Zoezi la kuweka kuponi likifanyika ili kushiriki droo ya kwanza ya Shinda Nyumba.

????????????????????????????????????

Wasomaji wakiendelea kuweka kuponi.

MAPEMA leo wasomaji wa magazeti ya Championi na Risasi Jumatano katika maeneo ya Vingunguti, Buza na Temeke jijini Dar es Salaam, wameonekana wakichangamkia magazeti hayo ili kushiriki droo ya kwanza ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba itakayofanyika kesho Alhamisi ambayo itaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd.

Katika bahati nasibu hiyo, msomaji anatakiwa kununua magazeti ya Global kadiri awezavyo na kukata kuponi, kisha kuijaza na kuituma kwa njia ya posta au kuifikisha moja kwa moja katika Ofisi za Global zilizopo Bamaga, Mwenge, Dar au hata kuwafikishia mawakala wa kuuza magazeti waliopo maeneo mbalimbali ya hapa nchini.

Droo ya kwanza ya bahati nasibu hiyo inatarajiwa kuchezeshwa kesho Alhamisi katika viwanja vya Mbagala Zakhem, Dar kuanzia saa sita mchana mpaka 12 jioni, huku zawadi mbalimbali kama simu za kisasa, dinner sets (vyombo vya ndani), bed sheets, TV, Ving’amuzi vya TING na pikipiki vitatolewa kwa washindi.

Masharti ya bahati nasibu hiyo hayaruhusu wafanyakazi wa Global, ndugu zao na watu walio chini ya umri wa miaka 18, kushiriki.

(Stori/ Picha: Denis Mtima/GPL)

Leave A Reply