Wasomaji Wafurahia Bei Mpya ya Sh. 500 ya Spoti Xtra
GAZETI la Spoti Xtra limekuja katika ujio mpya unaohusisha punguzo la bei ambapo kuanzia leo (Jumapili) linauzwa kwa Sh. 500 tu badala ya Sh. 800 iliyokuwepo awali na litakuwa linatoka mara mbili kwa wiki — Alhamisi na Jumapili.
Uzinduzi wa punguzo la bei umefanyika leo ambapo timu ya gazeti hilo la Spoti Xtra ilitembelea wasomaji wake maeneo ya Tabata-Kinyerezi, Segerea, Vingunguti, Ubungo, Mwenge na sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam ambapo magazeti yalitolewa bure.
Baada ya timu ya promosheni ya Spoti Xtra kutembelea wasomaji sehemu hizo, wasomaji hao walitoa pongezi kibao kwa maombi waliyoyatoa kuhusu kupunguziwa bei kwa gazeti hilo.
Ili kujishindia zawadi hizo, msomaji anatakiwa kununua gazeti la Spoti Xtra siku ya Alhamisi na Jumapili ambapo utatakiwa kujaza kupoeni iliyomo ndani ya gazeti hilo kwa kufuata maelekezo yaliyomo.
Uongozi wa Spoti Xtra umedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ya kuliboresha gazeti na wasomaji wake wakae mkao wa kupata burudani ya kutosha.
PICHA: RICHARD BUKOS | GPL
Comments are closed.