The House of Favourite Newspapers

WENZIO WANAJIZOLEA ZAWADI NA UWAZI, WEWE UNANGOJA NINI?

Hamis Mohammed akikabidhiwa kitita chake cha shilingi 50,000 na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Amrani Kaima (kushoto).

 

Mambo yamezidi kunoga kwenye ile Chemsha Bongo inayoendeshwa na Gazeti la Uwazi ambapo wasomaji mbalimbali wamejizolea zawadi za pesa taslimu pamoja na simu za mkononi.

    Mshindi wa simu, Maneno Masiku akikabidhiwa zawadi yake na mhariri wa Uwazi, Amran Kaima

Mpaka sasa wasomaji waliobahatika na Chemsha Bongo hiyo ni Masoud Kinyogoli wa Kitunda jijini Dar, Sabati Mghamba wa Same, Mohammed Elly wa Morogoro na Hamis Mohammed wa Magomeni waliojinyakulia shilingi 50, 000 kila mmoja huku Maneno Masika wa Mbagala jijini Dar akiwa mshindi wa kwanza wa simu ya kisasa.

Maneno Masiku (kushoto) Hamis Mohammed (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mhariri wa Gazeti la Uwazi, Amran Kaima

Sabati Mghamba alipokabidhiwa fedha zake alisema: “Ninachokipata kwa kununua gazeti la Uwazi kina thamani kubwa lakini sasa ukiongeza na pesa ambayo nimeshinda, nazidi kupata hamasa ya kusoma gazeti hili na magazeti mengine ya Global. Nawasihi tu watu wengine kununua gazeti hili kwani hakika linalainisha maisha yetu.”

Mshindi wa simu ya kisasa, Maneno Masiku alisema: “Kweli hii ni bahati yangu, nimekuwa msomaji mkubwa wa gazeti hili kwa muda mrefu, nilisikia furaha sana kupigiwa simu kuambiwa nimeshinda simu. Yaani nimeamini haya mashindano hayana upendeleo kabisa, kama una bahati yako unashinda tu.”

 

Akizungumza na mtandao huu, mratibu wa Chemsha Bongo hiyo, Elvan Stambuli alisema kuwa, katika kuhakikisha wasomaji wake wananufaika kwa kusoma Gazeti la Uwazi, wameamua kutoa zawadi hizo ikiwa ni sehemu ya kulainisha maisha yao.

Maneno Masiku akiifurahia zawadi yake ya simu ya kijanja.

“Gazeti la Uwazi kwa sasa limeboreshwa. Limesheheni habari na makala ambazo mtu akisoma anapata elimu lakini pia anaburudika. Mbali na faida hiyo, tumeanzisha chemsha bongo hii ambayo wasomaji wanajishindia pesa na simu kila wiki. Kikubwa nawasihi wasomaji wetu waendelee kununua gazeti kwani huenda wakabahatika,” alisema Stambuli.

Hamis Mohammed akifurahia mkwanja wake alioshinda

Ili ushinde ni rahisi, unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti la Uwazi, unakwenda ukurasa wa pili ambapo atakutana na kuponi yenye swali rahisi sana, atajibu kisha kutuma kwenda kwenye namba iliyowekwa, baada ya hapo atakaa mkao wa kusikilizia kupigiwa simu wakati wowote.

Kwa maelezo zaidi endelea kununu gazeti la Uwazi na magazeti mengine ya Global Publishers au piga namba 0658 798787!

Comments are closed.