Wasomi UDSM Wafanya Kongamano la Kuboresha Ubunifu wa Kibiashara

Dar es Salaam, 25 Machi 2025: Wasomi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wadau wake leo wameanza kongamano la siku nne ambalo litahusu masuala ya kuboresha kazi zao za ubunifu wa maendeleo ya kibiashara.
Katika kongamano hilo wadau wa chuo hicho akiwemo Mkuu wa Chuo hicho, Dkt Jakaya Kikwete, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Suleiman Jaffo wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hiyo.
Kongamano hilo limefunguliwa na Naibu Makamu Mkuu wa Utafiti (UDSM) Dkt. Nelson Boniface ambaye alianza na kuwapongeza washiriki wote waliofika kwenye kongamano hilo na kuwataja viongozi hao wakubwa kuwa nao wanatarajiwa kushiriki kongamano hilo.
Dkt. Nelson amewataka wabunifu hao kushirikiana kwa pamoja ili kupata suluhisho la kupambana na changamoto wanazokutana nazo kibiashara wanazozibuni na jinsi ya kuzilinda.
Katika kongamano wadau hao wanarajiwa kupata njia sahihi ya kuboresha kazi zao za kiubunifu ikiwemo kulinda haki miliki ya bunifu hizo. Alisema Dkt. Nelson.
Dkt. Nelson alimalizia kwa kusema kuwa wanawaalika wawekezaji ambapo wataangalia kazi zao na kuona jinsi gani wataingia nao ubia.
HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN /GPL