The House of Favourite Newspapers

Wassira Awasili Geita, Kuzindua Maadhimisho Miaka 48 Ya CCM – Video

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira amewasili mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine atazindua sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa CCM kwa Mkoa wa Geita.

BAada ya kuwasili mkoano humu Wasira alilakiwa na viongozi wa Chama wa mkoa huo pamoja na serikali wakiongozwa na Mkuu aa Mkoa wa Geita, kisha kupokea taarifa ya Chama na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kikao kilichofanyika ofifisi za CCM za mkoa huo.