WASTARA AANZISHA ‘PROJECT’ YA AKINA MAMA NA WATOTO

 MWANAMAMA kutoka tasnia ya sinema za Kibongo, Wastara Juma ameanzisha ‘project’ mpya ya kusaidia akina mama na watoto ili kutimiza ndoto yake ya kusaidia jamii aliyokuwa akiiota kila siku.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Wastara alisema yeye kama kioo cha jamii na mambo aliyopitia kwenye maisha, ameamua kuanzisha mradi huo alioupa jina Anzia Hapa Wastara akiwa na nia ya kuwasaidia akina mama na watoto.

“Kama unavyojua, mbali na kuwa msanii, mimi ni Balozi wa Wanawake Afrika kupitia Shirika la Wanawake na Watoto la Sweden (Asovu). Nimeamua kutimiza ndoto yangu ya kusaidia watoto na wanawake, pia kwa kupitia chama hicho ambapo rasmi nitakizindua Jumamosi (leo),” alisema Wastara.

Wastara alisema anafanya hayo kama njia ya kurudisha fadhila kwenye jamii ambayo imekuwa ikimsaidia kila anapokuwa kwenye wakati mgumu na katika kuhangaika kwake amegundia kuwa wapo wengi wanaohitaji msaada kama alivyokuwa yeye.

Loading...

Toa comment