The House of Favourite Newspapers

Wastara ampa ampa kichapo bondi

0

WASTARA2G.jpgStaa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma

Brighton Masalu

KAZI ipo! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadaiwa kumpa kichapo kikali aliyekuwa mwandani wake, Bond Suleiman baada ya kupatwa na kile kinachosemwa kuwa ni kupandisha majini.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kupandisha majini hayo kulitokana na jinsi ambavyo mwanaume huyo amekuwa akimtendea mpenziwe huyo, ambaye inadaiwa katika kupandisha huko, alitoa maelekezo ya namna anavyotakiwa kufanya.

IMG_2604Bond Suleiman.

“Nakuambia ilikuwa varangati siku hiyo, Wastara alipandisha majini akiwa na Bond, walikuwa wakijaribu kutatua mgogoro wao, lakini katika hali ya kushangaza, ghafla Wastara alibadilika na kuanza kusema hivyo kwa sauti tofautitofauti, kabla ya kumshushia kipigo,” kilisema chanzo chetu, kilichoomba hifadhi ya jina lake.

WASTARA-43.jpgWastara Juma na Bond.

Wastara alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alimtaka mwandishi wetu kuwasiliana na Bond, huku akidai hata kama ni kweli, hayo yanabaki kuwa maisha yao.

Kwa upande wake, Bond alikiri kutokea kwa sakata hilo na hadi wakati huo (Alhamisi) alikuwa Saadan, Bagamoyo katika Sober House akikamilisha zoezi la kupewa ushauri nasaha.

“Ni kweli niko huku, natekeleza adhabu niliyopewa na Wastara, ikiwemo kunyoa nywele, kupewa ushauri wa jinsi ya kuishi. Nimeachana na pombe, mirungi, shisha, kubadilisha wanawake na starehe nyingine za aina hiyo, sasa nimebadilika, sitamuumiza tena Wastara, zimebaki siku kama 6 nikamilishe zoezi hili,” alisema Bond.

Leave A Reply