The House of Favourite Newspapers

Wastara ateseka atamani kuua!

0

Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akisimulia kwa uchungu.

Mwandishi wetu

Hii ni habari ya kusikitisha! Staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma anadaiwa kuteswa na kitu kilichoitwa pepo mbaya ambaye humsababishia hasira kali hasa anapokosewa ambapo anapokumbwa na hali hiyo, hujikuta anataka kuua.

 

TUJIUNGE NA CHANZO

Sosi aliye karibu na staa huyo aliyezungumza na Ijumaa mapema wiki hii alinyetisha habari hiyo ambayo mbali na kumtesa Wastara, pia inaitesa familia yake kwani mara nyingi huamua kukaa mbali naye pindi anapokutwa na hali hiyo.Sosi huyo alinyetisha kwamba, kuna kipindi hali hiyo ikimkuta Wastara huwa na stress (msongo) wa mawazo.

HARUFU YA DAMU, KUTAKA KUUA MTU

Ilidaiwa kwamba, akiwa katika hali hiyo, Wastara huunguruma kama mtu aliyepandwa na kitu na husikika akisema kuwa anasikia harufu ya damu na kwamba anataka kuua mtu.“Yaani unaambiwa hali hiyo ikishamtokea huwa tunajifungia ndani na kumpisha anahangaika mwenyewe kwani tunahofia jambo baya la mauti,” alisema sosi huyo ambaye ni mtu wa ndani ya familia.

KUPOROMOSHA MATUSI

Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kutaka kuua, pia Wastara huporomosha matusi mfululizo ambayo akiwa kawaida hawezi kuyatoa, kitendo kinachoshangaza, kwani anaweza kutukana kuanzia asubuhi hadi jioni.

….Akizidi kusimulia.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WASTARA

Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimwendea hewani Wastara ili kujua kinachomsumbua ambapo alifunguka kwa masikitiko:
“Sijui ni nani amewafikishia habari hizi kwani zinanisikitisha sana lakini naomba watu watambue kuwa nina tatizo ambalo sijajua nitalimaliza vipi.“Wala huyo mtu hajakwambia uongo, ni kweli kwa sababu nina damu mchanganyiko na nikikasirika nyumba nzima wanajifungia ndani.“Ninajitahidi sana kujibadilisha ili niwe kawaida lakini inashindikana. Ndiyo maana huwa napenda kukaa kimya sana kwani najijua nina tatizo.

MCHANGANYIKO WA DAMU

“Nina mchanganyiko wa damu ya Kimasai, Kiarabu, Kinyamwezi, Kihindi, Kinyarwanda na Kigunya ndiyo maana nahisi nina tatizo kubwa ambalo naomba Mungu anitatulie.
“Kuna wakati huwa natamani kumpasua mtu pale anaponiudhi na asiamke kabisa ndiyo roho yangu inaridhika.

Akiwa na simanzi.

ALA MARA TANO, SODA ISHIRINI KWA SIKU
“Ninapokuwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi huambatana na ‘stress’ zilizonizidi, huwa najikuta nakula sana kama mara tano kwa siku na huwa nakunywa soda kama ishirini hivi.“Mtu akiniona nanenepa ni kwa sababu ya stress za maisha ndiyo husababisha hali niliyonayo.

AJITAHIDI KUSALI

“Huwa najitahidi kusali sana ili nione kama hali hii itaniondokea, naamini ipo siku nitakuwa sawa na matatizo yote yataisha. Pia ni jambo la kuombewa sana dua.

TUJIKUMBUSHE

Wastara amekuwa akikumbwa na mikasa ya kila aina kama ajali za mara kwa mara hivyo kujiona mwenye mikosi ambapo mashabiki wake wamekuwa wakimshauri kusali sana ili aepukane na mikosi hiyo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply