The House of Favourite Newspapers

WASTARA, MAMA SOPHIA: ASANTENI SANA GLOBAL

Wastara akionyesha mguu wake uliokatwa.

KAMPUNI ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Risasi na Ijumaa Wikienda imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii tangu kuanzishwa kwake. Wengi wamepata nafasi ya kupaza sauti zao kutokana na matatizo yanayowakabili na hatimaye kusikika na kusaidiwa.

 

Idadi ya walionufaika na kampuni hii ni ndefu sana. Wapo wagonjwa ambao walikosa tumaini la kuendelea kuishi lakini baada ya kuandikwa kupitia magazeti haya, wamepata misaada ya matibabu na sasa wanaendelea na maisha yao.

…Akifanya mahojiano na Global TV.

 

Mbali na wale ambao walisaidiwa siku za nyuma, hivi karibuni kampuni hii kupitia magazeti yake mawili, Amani na Risasi Jumamosi yamefanya kazi kubwa ya kuwapazia sauti watu wawili ambao ni walemavu wa miguu na sasa wote wanatabasamu baada ya kupata msaada.

 

Siku chache nyuma, Gazeti la Risasi Jumamosi liliandika kwa mara ya kwanza juu ya tatizo ‘siriasi’ alilokuwa nalo staa wa fi lamu Bongo, Wastara Juma ambaye alikuwa akisumbuliwa na mguu, ule ambao alikatwa miaka kadhaa nyuma baada ya kupata ajali.

Ngusa Samike ambaye ni Katibu wa Rais akiwasilisha mchango wa Sh. milioni 15 kwa mwigizaji Wastara Juma kutoka kwa Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli kwa ajili ya matibabu.

 

Wastara aliongea na gazeti hilo kwamba, alikuwa akihitaji msaada kwa ajili ya kwenda kufanyiwa upasuaji wa mguu huo ambao ulikuwa kwenye hali mbaya.

 

Mara baada ya kuandika habari hiyo, mbali na Makamu wa Rais, Samia Suluhu kuwahi kumpa msaada wa matibabu, taarifa pia zilimfi kia Rais John Magufuli ambaye alituma wawakilishi wake ambao walimpelekea Wastara kiasi cha shilingi milioni 15 ambazo zilimuwezesha kwenda India kwa matibabu.

Sidonia Ntibashigwa ‘Mama Sophia’ akionyesha mguu wake uliokatwa.

Akizungumzia msaada huo wa rais, Wastara alilishukuru Gazeti la Risasi Jumamosi kwa kufi kisha habari zake kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa nchi ambao walijitolea kufanikisha matibabu yake.

 

“Nawashukuru sana Global, hakika mchango wenu kwa jamii ni mkubwa, naamini bila ninyi huenda rais na watu wengine wasingepata taarifa zangu, Mungu awabariki sana,” alisema Wastara alipokuwa akiondoka kuelekea kwenye Hospitali ya Saifee nchini India kwa matibabu.

Msaidizi wa Makamu wa Rais, Nehemia Mandia akimkabidhi baiskeli ya kutembelea Bi.  Sidonia Ntibashigwa.

 

Wakati Wastara akielekea zake India, Gazeti la Amani nalo lilipokea taarifa za kuwepo kwa mama mmoja aliyefahamika kwa jina la Sidonia Ntibashigwa ‘Mama Sophia’ mkazi wa Salasala jijini Dar ambaye naye alikuwa na tatizo kama la Wastara.

 

Mama huyo alieleza kuwa, mwaka 2016 alipata ajali ya kugongwa na lori na kukatwa mguu wa kulia na sasa anahitaji msaada kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wa kushoto.

Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne aliwaomba wasamaria wema kumsaidia ili apate matibabu lakini pia kiti cha matairi ili kiweze kumsaidia.

Siku chache baada ya gazeti hilo kuandika habari ya mama huyo, walijitokeza watu kadhaa wa kumsaidia pesa kidogo lakini baadaye Makamu wa Rais, Samia Suluhu naye aliguswa na tatizo hilo ambapo aliwatuma wasaidizi wake kumpelekea msaada wa kiti mama huyo.

 

Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais, Nehemia Mandia alisema; “Mheshimiwa Makamu wa Rais ameguswa na suala lako ambalo liliandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na ajali. Kwa hiyo kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa ajili ya wewe kufanya shughuli zako ndogondogo unazoweza kufanya.”

 

 

Baada ya mama huyo kupokea msaada huo alizungumza na mwandishi wetu na kueleza kuwa, analishukuru sana Gazeti la Amani ambalo ndilo lililoandika habari hiyo na hatimaye makamu wa rais kusikia na kuguswa.

MAMA ALIA… NATESEKA ZAIDI YA WASTARA

“Sijui niwashukuru vipi jamani, asanteni sana. Mama Samia mlivyoandika ile habari aliguswa na kanipatia msaada wa kiti cha magurudumu. Asanteni sana ila bado nahitaji pesa za kuutibia huu mguu mwingine mbali na huu uliokatwa,” alisema mama huyo.

Wastara baada ya kurejea nchini jana Alhamisi.

Hivyo ndivyo Global inavyosaidia jamii. Kama umeguswa na tatizo la Mama Sophia na ungependa kuungana na Mama Samia kumnusuru mama huyo, unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0653659379.

 

NA MWANDISHI WETU

VIDEO; MSIKIE WASTARA AKIFUNGUKA

 

Comments are closed.