The House of Favourite Newspapers

Wastara: Nakuja kivingine

0

wastara788Msanii wa filamu Wastara Juma.

Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu Wastara Juma ambaye hivi sasa anapata matibabu ya mguu wake nchini India, amedai akirejea nchini, atakuja kivingine katika kazi zake za uigizaji.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa huko, Wastara alisema anam shukuru Mungu kwani anaendelea vizuri na matibabu, lakini akawaahidi mashabiki wake vitu vipya kwani safari yake huko imemuo ngezea ubunifu.

“Yaani nikirudi Bongo naamini nitakuwa niko fiti na nitafanya makubwa kwa kutoa filamu kali zenye ubunifu mkubwa tofauti na zamani hivyo mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema
Wastara.

Leave A Reply