The House of Favourite Newspapers

Wastara umekiri starehe zimekuponza, badilika kweli!

0

IMG382KWAKO dada yangu Wastara Juma Kilowoko. Habari za siku? Vipi unaendeleaje na shughuli zako? Bila shaka Mungu anaendelea kukupigania, ni vyema na haki ukaendelea kumtumainia yeye, maana ndiye muweza wa yote.

Ukitaka kujua afya yangu, mimi ni mzima wa afya. Naendelea na harakati zangu kama kawaida. Mungu ni mwema pia, anaendelea kubariki kazi za mikono yangu. Mkono unakwenda kinywani kama kawaida, naendelea kumtumainia yeye!

Dhumuni la barua hii, kwanza ni kukusalimu. Lakini baada ya salamu, nina jambo nataka nikueleze maana kutokana na ubize wa kazi zetu, wakati mwingine unapita muda mrefu pasipo kuonana na kwa ubize wa mjini, basi si vibaya ukapokea ujumbe wangu kupitia barua hii.

Kikubwa hasa nilichotaka kukueleza ni kuhusu suala la wewe kukiri kwamba starehe zimekuponza. Nilisoma wiki iliyopita katika moja ya magazeti Pendwa. Ulionesha kwamba hukukubaliana na hali uliyonayo na ukaona uendelee kufanya starehe za mjini.

Ulitamani maisha yale ya awali ambayo ulikuwa ukiishi ukiwa na miguu yako yote miwili. Muziki ulikukaa kwenye damu, hukukubali kupitwa na matukio ya kiburudani.

iyo inaweza kuwa sababu kubwa ya kuusababishia mguu wako matatizo zaidi.
Wewe mwenyewe ni shahidi wa matokeo ya mishemishe ulizokuwa unazifanya.

ikakusababishia uende kufanyiwa tena upasuaji nchini Kenya. Kwanza nikushauri kwamba kutokana na mitihani uliyopitia maishani, sitegemei sana uwe mtu wa kujisahau.

Ninapata shida kidogo ninapokusikia ukifanya starehe zile ambazo zinapaswa kufanywa na vijana wadogowadogo kama kina Mo Music. Hawa ambao ndiyo kwanza wanachipukia kwenye umaarufu, si wewe mama. Wewe una uzoefu na maisha.

Umepitia ndoa mbili tofauti. Umepata majaribu makubwa sana. Yakupasa umshukuru Mungu kwa kuweza kukuvusha huko. Mungu anakupenda ndiyo maana amekupigania hadi sasa upo. Jina lako ni kubwa katika sanaa, fanya sanaa ya kweli na Mungu atabariki kazi ya mikono yako.

Wewe ni mpambanaji kila mtu anatambua. Achana na hizi starehe sijui za kunywa pombe au kutembea na vijana wa mjini. Kwa kuwa umesema kweli umejitambua, badilika kweli na usipoteze sifa yako ya upole. Usipoteze nafasi yako ya muigizaji anayejiheshimu.

Wewe ni miongoni mwa waigizaji ambao wanafahamika kwa kujiheshimu, kujitambua. Usikubali kupelekwa na kasi ya starehe, umri pia si rafiki kwako. Huu ni wakati wa kuzidi kudhihirisha kipaji chako kwa kuwafundisha waigizaji wachanga sanaa ni nini.

Una watoto watatu sasa wanakutegemea. Fanya kazi kwelikweli. Naamini kwa msaada wa Mungu utawalea vizuri na watasoma vizuri. Wafundishe maadili mema, waje kuiga mazuri yako ambayo utakuwa umewafundisha.

Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa na utabadilika kweli. Mungu akusimamie dada yangu.
Ni mimi kaka’ko;
………………
Erick Evarist.

Leave A Reply