The House of Favourite Newspapers

Watafiti: Nyimbo za Eminem Zinaongeza Spidi ya Mazoezi

0

 Rapa maarufu wa Marekani, Mathew Matthers Eminem.

UNAWEZA kudhani ni utani lakini hili limetokea nchini Uingereza baada ya jopo la watafiti nchini humo kutoa utafiti wao kuwa nyimbo za rapa maarufu wa Marekani, Mathew Matthers zinaongeza morali ya mazoezi na spidi kwa wanamichezo.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Hartpury, Uingereza walidai kutumia miezi mitatu wakichunguza matokeo ya kisaikolojia na kifizikia kwa wanamichezo kutokana na aina mbalimbali ya nyimbo za wanamuziki wanazozisikiliza pindi wanapofanya mazoezi ambapo walimtumia muogeleaji maarufu wa Uingereza, Ben Hooper ambaye kila aliposikilizishwa nyimbo za Eminem kama vile;Lose Yourself na Without Me alionesha kuongeza spidi na kuvumilia mazoezi kwa kipindi kirefu zaidi ya kawaida yake.

Hata hivyo, watafiti hao walisema kuwa tofauti na nyimbo za staa huyo nyimbo za mwanamuziki nguli wa Reggae, Bob Marley zimekuwa zikishusha morali ya mazoezi kwa wanamichezo hivyo wanamichezo wameshauriwa kusikiliza nyimbo za Eminem ili kujiweka fiti zaidi.Utafiti huo tangu kutolewa kwake umeonekana kukubalika sana na wanamichezo wengi nchini Marekani na Uingereza.

Leave A Reply