The House of Favourite Newspapers

Watahmini wa Madini Wazidi Kusota Rumande

0

KESI inayowakabili Mkurugenzi wa Tathmini, Archad Alphonce Kalugendo na Mthamini wa Serikali wa Madini, kutoka iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Edward Joseph Rweyemamu, imeahirishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutokuwepo.Watu hao wanatuhumiwa kwakuisababishia serikali ya hasara ya zaidi ya Sh. bilioni 2.

Awali  watuhumiwa walisomewa shtaka la uhujumu uchumi ambapo hawakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za namna hiyo.  Walisomewa mashtaka  mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage na Wakili wa Serikali, Paul Kadushi. Kalugendo na Rweyemamu wote ni waajiriwa wa Wizara ya Nishati na Madini.

Kadushi alidai kati ya Agosti 25 na ,31, 2017 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na Shinyanga washtakiwa hao kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini walisababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, washtakiwa hawakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu. Upande wa mashtaka alidai kuwa upelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Hakimu Mwijage aliwaeleza washtakiwa hao kuhusu dhamana mawakili wao wafuatilie Mahakama Kuu.

Kwa upande wa Wakili  Ludovic Nickson anayemtetea mshtakiwa Kalugendo aliomba upelezi ukamilike haraka na kwa upande wa dhamana watatakiwa kwenda Mahakama Kuu. Wakili wa mshtakiwa wa pili, Rweyemamu, Nehemiah Nkoko naye adai kuwa washtakiwa wamekaa polisi kwa muda wa takribani wiki mbili anadhani upelelezi utakuwa umekwishakamilika.

Hivyo aliomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka. Wakili wa Serikali, Kadushi alidai kuwa watahakikisha wanakamilisha upelelezi kwa wakati. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wamepelekwa rumande.

NA DENIS MTIMA | GPL

Tazama ‘Mauno’ ya Masogange Alipofika Kisutu Leo

Leave A Reply