The House of Favourite Newspapers

Watangazaji 8 wa Runinga Wanawake Wasimamishwa Kazi Kisa Unene

0

khadijaShirika la Utangazaji la Misri ‘Egyptian Radio and Television Union (ERTU)’ limewasimamisha kazi watangazaji wake wanane wa televisheni wa kike kwa madai kuwa ni wanene wa kupindukia.

ERTU limewapa  muda wa mwezi mmoja watangazaji hao kupumzika kazi, wakae nyumbani huku likiwaagiza kuhakikisha kuwa wanakula vyakula vyenye lishe bora ili wapungue unene na kuwa na muonekano unaovutia kabla hawajaonekana tena luningani.

Mmoja kati ya watangazaji hao waliosimamishwa kazi, Khadijah Khattab, anayeongoza kipindi kwenye televisheni ya Channel 2, amesema amehudhunishwa kitendo hicho na kuongeza kuwa anataka watazamaji waangalie vipindi vyake alivyofanya hivi karibuni kisha watoe maoni yao kama kweli yeye ni mnene kiasi hicho mpaka asimamishwe kazi.

Mtangazaji mwingine alisema bora angeachwa akashughulikia tatizo la unene wake yeye na familia yake na sio kumsimamisha kazi na kumwanika kwenye mitandao ya kijamii ilivyofanyika.

Kituo cha Haki za Bianadamu nchini humo kimelaani kitendo hicho na kueleza kuwa jambo hilo ni udharirishaji wa wanawake na ukiukwaji mkubwa wa katiba ya nchi ilihali ERTU inaongozwa na mkurugenzi ambaye pia ni mwanamke.

Leave A Reply