The House of Favourite Newspapers

Watano wauawa kwa risasi Marekani

0

usa

TAKRIBANI watu watano wameuawa wakati wa ufyatuaji wa risasi uliotokea karibu na mji wa Pittsburg uliopo kwenye Jimbo la Pennsylvania nchini Marekani.

Maofisa wa polisi wameeleza kuwa watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi kwenye sherehe moja ambapo pia watu wengine watatu walijeruhiwa.

Watu wanne kati ya waliouawa walikuwa ni wanawake huku watu waliofanya mauaji hayo wakiwa bado hawajafahamika.

Misururu ya mauaji kwa kutumia bunduki imechangia suala la umiliki wa bunduki kuwa mjadala mkubwa nchini Marekani.

Watu wanne walikufa eneo la mkasa huku mmoja akiaga dunia alipofikishwa hospitalini. Wanaume wawili waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.

Chanzo: BBC

Leave A Reply