Watanzania 9 Wauawa Mpakani na Msumbiji, Sirro Atoa Tamko – Video

RAIA tisa wa Tanzania  na raia wawili wa Msumbiji wameuawa na watu wasiojulikana huku Watanzania wengine sita wakijeruhiwa vibaya katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefika mkoani Mtwara kufuatilia tukio hilo lililotokea Juni 26, 2019,  na kusema msako unaanza mara moja kwa kushirikiana na serikali ya Msumbiji ili kuwakamata watu waliohusika na mauaji hayo.

 

Wakizungumzia tukio hilo,  majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Ligula wamesema kuwa watu hao waliofanya mauaji walikuwa saba na waliwalaghai wananchi kwa kuitisha mkutano na kuanza kuwashambulia.

 

Majeruhi hao wameiomba serikali kuhakikisha inawakamata wauaji hao. Mauaji hayo yalitokea wakati Watanzania hao kutoka Kijiji cha Kihamba upande wa Mtwara wakiwa kijijini hapo kwa shughuli za kilimo.

Majeruhi mauaji ya watanzania 9 Msumbiji wafunguka. Siro azungumza Mtwara

TBC1: SAKATA la MAUAJI Mtwara, MASHUHUDA Wasimulia Mazito, IGP Sirro Atinga!

Loading...

Toa comment