The House of Favourite Newspapers

Watanzania fanyeni kazi, achene kulalama!

magufuli-640x350

Vijana watanzania wenzangu tufanye kazi na kumunyenyekea Mungu pekee ili tupate kutimiza kusudi lake la kutuleta Duniani ili kuondokana na malalamiko yakuwa hakuna mvua nchini tukibaki kuilaumu serikali pasipokuangalia maovu yetu sisi na kuyakemea.
Vijiji vyetu vina idadi kubwa ya watu hata zaidi ya elfu mbili lakini vinabaikia kulalamika kuchimbiwa visima badala ya kukaa wao wenyewe na kujumuika kwa pamoja ili kufanikisha zoezi la visima na kama hiyo haitoshi kufuga mifugo zaidi ya uwezo wao na kulalamika kuwa hakuna eneo la kuchungia.

“Niwambie ndugu zanguni hakuna inchi bora kama yetu Tanzania ambayo tumebarikiwa kumpata rais bora, mpenda haki, anayetetea wanyonge,hakika tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kiongozi wetu huyu,”
“Tusiendelea kumbeza rais wetu Magufuli kwani ni tunu letu tumepewa na Mungu,wanasiasa na baadhi ya watu wengine wamuache afanye kazi yake na si kupiga porojo,”.
Ukiangalia mataifa kama ya Misri,India na nchi za kiarabu hazina ardhi kubwa kama ilivyo Tanzanialakini haijawahi kusikika kuwa zimekubwa na balaa la njaa, wakati wana watu wengi hivyo ni Dhahiri ya kuwa sisi tunapenda kulalamika.
Kazi kubwa ya serikali ni kuhakikisha inarekebisha miundombinu ya maeneo pamoja na mambo mengine lakini siyo kugawa vyakula pasipokuwa na tatizo.
Imeandaliwa na mwanakijiji mmoja kutoka Wilaya ya Igunga,Tabora.
Asiyefanya kazi na asile.

Comments are closed.