Watanzania Walisifia Gazeti la Michezo la Spoti Xtra

Wakazi wa Sinza jijini Dar es Salaam wakisoma gazeti la michezo la Spoti Extra la leo Jumapili.
Ofisa Masoko wa Spoti Xtra, Jimmy Haroub, akimwonyesha msomaji uhondo uliomo katika gazeti la Spoti Extra leo eneo la Uwanja wa Taifa.
Wasomaji wakisoma data za michezo zilizomo ndani ya gazeti la Spoti Xtra wakiwa na Jimmy Haroub eneo la Keko, Dar.
Msomaji aliyekutwa akisoma gazeti la Spoti Extra eneo la Keko akiwa na mwenzake leo.

PROMOSHENI ya gazeti la Spoti Extra linalotolewa na kampuni ya Global Group imeendelea leo maeneo ya Sinza, Mabibo, Soko la Ndizi, Kigogo, Keko na Tandika Sokoni jijini Dar es Salaam kuchukua maoni ya wasomaji na kuwaeleza faida za kusoma gazeti hilo ambalo hutoka kila Jumapili.

Wasomaji waliofikiwa leo wamelisifia gazeti hilo wakisema ni gazeti bora kwa siku za Jumapili ambalo linakata kitu kwa kile walichokuwa wanakikosa siku hiyo kwani limesheheni data mbalimbali za michezo ndani na nje ya Tanzania.

Vilevile, wameomba liendeleze ubora wake zaidi ili kuweza kuteka mioyo ya Watanzania wengi wapenda michezo na habari nyingine za burudani.  Pia wamesema kwamba ni gazeti pekee nchini Tanzania ambalo linafanana na magazeti ya nje ya michezo.

Kwa ambao hawajaliona gazeti hili ni vyema wakalitafuta sasa kwani liko mitaani kila Jumapili kwa bei ya Sh. 500 tu.  Ni gazeti lililosheheni uhondo mtupu kukata kiu yoyote ya michezo na burudani.

(PICHA: RICHARD BUKOS/GPL)

Loading...

Toa comment