Watanzania wawili wakamatwa kwa kuingiza bangi Kenya

WATANZANIA wawili, Annah Mwisawa, 34, na  Jackson Josephat, 20, wamekamatwa nchini Kenya kwa kuingiza bangi nchini humo yenye thamani ya Sh. 500,000 za Kenya.

Watu hao walikamatwa na polisi wakiwa na bangi hiyo ikiwa imefichwa katika magunia matatu katika kisiwa cha Remba, katika Ziwa Victoria.

Mkuu wa polisi wa Suba Kaskazini,  AP Kamanda Elias Wasonga, amesema polisi waliwakamata watuhumiwa hao kutokana na kudokezwa na raia.

“Watuhumiwa walikuwa wakitumia mtumbwi wa kuvulia samaki ili waonekane walikuwa wakifanya kazi halali,” alisema Wasonga.

 

Wakati huohuo, polisi nchini humo imesema itawakamata raia wa Kenya wanaokula njama na wageni ili kuingiza bidhaa haramu nchini humo.

Loading...

Toa comment