The House of Favourite Newspapers

Watatu Mbaroni Kujiunganishia Umeme wa TANESCO

0

WATU watatu akiwemo mfanyabiashara, Gaston Masika (58) na wenzake wawili wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

 

Washtakiwa wengine ni Gerald Mmasi (58) mkazi wa Mvomero, mkoani Morogoro na Freeman Shirima (48) mkazi wa Mbezi Juu.

 

Wamesomewa mashtka yao Mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo, na wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali Mkuu, Marterus Marandu, akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Wankyo Simon na Ashura Mzava.

 

Katika shtaka la kwanza, wakili Simon amedai Februari 2, 2016,  eneo la Mwenge, Masika na Mmasi kwa makusudi waliingilia miundombinu iliyowekwa kwa ajili ya kusambaza huduma za umeme.

 

Shtaka la pili, ni kwamba April 11, 2016, eneo hilo, Masika na Mmasi, waliiba umeme kwa kuchepusha kutoka Tanesco, kwa matumizi yao na hivyo kuisababisha hasara Tanesco ya Sh 10,803,144.

 

Simon amedai pia, Agosti 6, 2020 katika eneo la Mwenge, Shirima aliingilia miundombinu iliyowekwa kwa ajili ya kusambaza umeme, kwa kuchepusha au kuhamisha umeme kutoka Tanesco na kuunganishia katika mita ambayo ilikuwa haipo katika matumizi ya umeme.

 

Kesi hiyo imeahirishwa na upelelezi haujakamilika na Hakimu Mwaikambo,  ameahirisha kesi hiyo hadi  Septemba 15, 2020, na washtakiwa wamerudishwa rumande.

 

Leave A Reply