Watatu wa Familia Moja Wafa kwa Kula Uyoga

#BADNEWS: Katika hali ya kustaajabisha, watoto watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kudaiwa kula uyoga unaodhaniwa kuwa na sumu katika eneo la Igombanilo, Nzega Mkoani wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema waliokula chakula hicho ni mama na watoto wake ambapo mpaka sasa mama na mtoto mmoja wanaendelea vizuri na wameruhusiwa kutoka Hospitali.

Kamanda Abwao amewataja waliofariki dunia ni Happiness Greyson, Annastazia Greyson na Maria Greyson.701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment