The House of Favourite Newspapers

Watatu Wafariki, 66 Wajeruhiwa kwenye Ajali ya Treni

0

TRENI ya abiria iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kuelekea Bara (Mwanza, Mpanda na Kigoma kupitia Tabora) imepata ajali Wilayani Bahi umbali wa kilometa 40 kutoka Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amethibitisha.

 

“Treni ilikuwa na Watu zaidi ya 700, kuna mvua zinanyesha sana, bado hatujajua chanzo cha ajali ila kichwa kimeanguka, taarifa za awali zinaonesha Mfanyakazi wetu mmoja amefariki na abiria wawili wamefariki, nilikuwa likizo nimeikatisha naelekea eneo la tukio”- Kadogosa

 

“Tunaandaa Mabasi ya kwenda kuchukua abiria pale wawapeleke Manyoni, kuna Treni yetu ya abiria inatoka Bara, wanaoendelea na usafiri Bara waingie huko waendelee na safari, na waliokuwa wanatoka Bara kuelekea Dar Es Salaam waingie kwenye Mabasi wawalete DSM”-Kadogosa.

Aidha Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) imesema, ajali  lilitokea Maeneo ya Kigwe-Bahi umbali wa Kilomita 508 Kutokea Dar Es Alaam na Kilomita 58 Kutokea Dodoma, Treni hiyo ilikuwa inatokea jijini Dar Es Salaam ikielekea Mikoa ya Tabora, Katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza  ikiwa na Abiria wapatao 720.

 

Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na Kuondoka Dodoma majira ya Saa 11:40 Jioni. Treni hii iliwasili katika kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 Jioni na Kuondoka saa 12:27 Jioni

Mpaka sasa Majeruhi ni 66 na waliopoteza maisha ni watatu (3), akiwemo mtoto mmoja (1) na watu wazima wawili (2) majeruhi wamekwisha chukuliwa eneo la Tukio na wanaendelea na matibabu katika Hospitali za Bahi na hospitali ya Mkoa wa Dodoma, uchunguzi wa Chanzo cha ajali unaendelea kufanyika na Shirika litaendelea kutoa Taarifa.

 

Leave A Reply