The House of Favourite Newspapers

Watatu Wafariki Dunia Kwa Kuangukiwa na Ndege – Video

0

Watu watatu akiwemo dereva bodaboda mmoja na abiria wake na mwalimu, wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ndege ndogo, tukio lililotokea katika Kijiji cha Kwachocha, Malindi nchini Kenya.

Ndege hiyo iliyokuwa kwenye safari ya kawaida ya mafunzo, inadaiwa kuwa ilipata hitilafu ya kiufundi, na kuilazimu kutua katika barabara kuu ya Malindi-Mombasa, na kusababisha maafa hayo.

Kulingana na ripoti ya polisi, ndege hiyo aina ya Cesna 172 ilikuwa ikitoka katika Uwanja wa Ndege wa Malindi kuelekea Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi ilipopata matatizo ya kiufundi.

Rubani wa ndege na wahudumu wengine akiwemo aliyekuwa akipatiwa mafunzo waliokolewa na kukimbizwa katika Hospitali ya Tawfiq, Malindi huku abiria mmoja akiteketea kiasi cha kutotambulika.

Leave A Reply