The House of Favourite Newspapers

Watatu Watimka Azam FC, Yupo Dube

0

JUMLA ya wachezaji watatu wanatarajiwa kuondoka katika kikosi cha Azam FC kwenda katika timu ya taifa
ya Zimbabwe kushiriki
michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).


Wachezaji hao ni beki wa
kushoto, Bruce Kangwa, kiungo Never Tigere na mshambuliaji Prince Dube. Nyota hao huenda wakosekana katika michezo baadhi ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA kutokana na
kuwepo katika majukumu ya
timu ya taifa.


Kwa mujibu wa mtandao wa
nchi ni Zimbabwe, wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha awali kuelekea michuano
ya AFCON itakayoanza Januari
9 hadi Februari 6, 2022 nchini Cameroon.


Mastaa hao wa Azam,
wanatarajiwa kuingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya mchujo wa mwisho utakaowawezesha kuwepo sehemu ya kikosi cha Zimbabwe kitakachokwenda Cameroon katika michuano
hiyo.


Ofisa Habari wa Azam FC,
Thabiti Zakaria, alithibitisha hilo kwa kusema: “Ni kweli wachezaji hao wameitwa katika kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Zaimbabwe, hivyo muda wowote watajiunga nayo.”

STORI NA WILBERT MOLANDI, DAR

Leave A Reply