Watatu Yanga Kuikosa Rivers

Wakati Yanga wakijiandaa na mchezo huo, taarifa zilizopo ni kwamba wanatarajia kuwakosa wachezaji wao watatu ambao ni Mapinduzi Balama, Yassin Mustapha na David Bryson ambao wote wanasumbuliwa na majeraha.

 

“Juzi wachezaji wetu walipewa mapumziko ambayo yaliisha juzi Jumatatu) na jana Jumanne wamerejea kambini.“

 

Katika kuelekea mchezo huo tunatarajia kuwakosa wachezaji wetu watatu ambao wote wana majeraha. Kuna Yassin na Balama ambao wanafanya mazoezi binafsi na Bryson aliyeanza mazoezi ya jumla na wenzake lakini hana fitinesi ya kutosha, hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi chetu,” alisema Saleh.

 

RIVERS WATUA
Mchana wa juzi, kikosi cha Rivers United kiliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar tayari kwa kukabiliana na Yanga Jumapili hii.

WILBERT MOLANDI, DAR701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment