Wateja wa DStv waula kwenye Promosheni ya “Tia kitu pata vituz” 

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akichezesha droo ya kupata washindi wa huku afisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Jehud Ngolo (kulia) akifuatilia kwa makini. Kushoto ni Benson Urio wa kitengo cha Teknohama cha DStv.

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (Katikati) Akizungumza kwa simu na moja ya washindi wa promosheni hiyo. 

 

Wateja 15 wa DStv wameibuka washindi wa wiki ya kwanza ya promosheni ya “Tia kitu pata vituz” inayoendeshwa na MultiChoice Tanzania. Kampeni hiyo itakayodumu kwa wiki 8, itakuwa ikitoa washindi 15 kila wiki hivyo jumla ya washindi 120 katika kipindi chote cha promosheni.

 

 

Promosheni hiyo ni kwa wateja wote wa DStv ambao watalipia vifurushi vyao kabla havijakatika. “Mteja yeyote wa DStv atakayelipia kifurushi chake kabla hakijakatika moja kwa moja anaingia katika droo na ana fursa ya kujishindia kifurushi chake kwa muda wa miezi miwili” alisema Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo wakati wa kufanya droo ya wiki ya kwanza ya promosheni hiyo.

 

 

Akizumgumza baada ya kujuzwa kuhusu ushindi wake huo Neema Nsabimana ambaye ni mteja wa DStv aliyepo mkoani Mwanza amesema kuwa amefurahi sana kuibuka mshindi kwani yeye ni mpenzi wa vipindi DStv hivyo waendelee kuwajali wateja wake hivyo hivyo.

 

 

Naye Lulu Mahamba wa Dar es Salaam, amefurahishwa na zawadi hiyo na kueleza kuwa kweli DStv inawakumbuka wateja wake.

Toa comment