The House of Favourite Newspapers

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa  Mfumo wa Kielekroniki Serikalini (GePG)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektroniki.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

 

WATEJA wa Kampuni ya Tigo  wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

 

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa  Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta  faida  nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali

 

“Mfumo wa GePG,  pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema Manyama

 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo  mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti

 

Aliongeza “Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,”

 

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara ya Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300.

 

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala.

 

Comments are closed.