The House of Favourite Newspapers

Wateja wa Y9 Microfinance Waongezewa Dau la Mkopo

0
 Taasisi ya kifedha ya Y9 Microfinance imeendelea na utaratibu wake wa kukabidhi zawadi kila wiki ambapo wiki  hii wamekabidhi zawadi ya pikipiki mbili kwa washindi wa Droo ya nne kwa wakazi wa Njombe na Songea.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji wa Taasisi ya  Y9  Microfinance  Bw. Fredrick Mtui amesema kuwa taasisi ya Y9 ilianzishwa mahususi kuwasadia na kuinua mitaji ya wale wenye kipato cha chini na watanzania wote nchini.
Lengo kuu la Y9 Microfinance ni kuhakikisha kila mtanzania anapata fursa hii kwa kuhakikisha anapakua app ya Y9 Microfinance na kupata huduma ya tatu ambazo ni  mkopo wa fedha taslimu.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Taasisi ya Y9 Microfinance, Sophia Mang’enya ambaye pia alieleza kuwa hii ni fursa kubwa sana kwa watanzania kwani Taasisi ya Y9 umeongeza pia kiwango cha mkopo pia siku za kulipa deni la mkopo
Mang’enya ameeleza kuwa jwasasa mteja wa Y9 anaweza kukopa kuanzia elfu mbili hadi laki tatu na muda wa kurejesha ni siku 9 ambapo awali kiwango cha juu kilikuwa laki moja na muda wa kurejesha ni siku tatu
Ameeleza kuwa nia na madhumuni ya kuongeza kiwango cha mkopo nikuridhishwa na mwenendo mzuri wa ulipaji kwa wateja wao hivyo amewasihi watanzania wachangamkie fursa hii ambayo haina mashart magumu.
 amewapongeza washindi wote  kwa kujiunga na huduma zao na kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo simu, pikipiki vilevile ameongeza kwamba kwenye droo ya mwisho ambayo itanyika katikati ya mwezi  Disemba  kutakuwa na  zawadi  kubwa zaidi ya gari aina ya Toyota IST. na zawadi nyengine kemkem
Alisema kuwa washindi hao wameshinda zawadi hizo baada ya kupakuwa App  yetu na kukopa kupitia app  na kurejesha mikopo yao ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu zetu.
 Alisema kuwa zawadi bado zipo nyingi kikubwa Watanzania kuendelea kutumia humu zetu ili kujishindia zawadi.
Leo pia tumechezesha droo ambapo tumepata washindi  wawili ambao ni Riziki Makame ambae amejishindia pikipiki ya matairi mawili  pamoja na mkazi wa Arusha Bw. Peter ambae amejishindia simu janja.
Leave A Reply