The House of Favourite Newspapers

WATENDAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAKUTANA KUJADILI RASIMU YA MWONGOZO WA MPANGO WA RASILIMALI WATU ‘HRPG’

Mtendaji wa Mahakama ya Rufani (T), Bw. Sollanus Nyimbi akifungua rasmi Mafunzo ya siku tatu (3) ya kujadili rasimu ya Mpango wa Rasilimali watu ya Mahakama ya Tanzania yaliyoshirikisha Watendaji wa Mahakama kutoka Kanda, Mikoa na Divisheni mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya Maafisa kadhaa wa Mahakama. Lengo la Mafunzo hayo ni kuwapitisha Watendaji hao katika rasimu hiyo ili kupata maoni ili kuiboresha zaidi kabla ya utekelezaji wake kuanza rasmi. Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Kituo cha Mafunzo Kisutu uliopo eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu-Dar es Salaam yamefunguliwa rasmi Juni 03, 2019.
Sehemu ya Maafisa na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Sehemu ya Maafisa na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Maafisa na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakimsikiliza mgeni rasmi alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Edith Rwiza (aliyesimama) akiwasilisha Mada katika mafunzo hayo. Kwa mujibu wa Mwezeshaji Mpango wa Rasilimali watu ‘HRP’ unawezesha Taasisi kujua idadi kamili ya uhitaji wa Rasilimali watu kwa Kada mbalimbali na vilevile husaidia kujua ni Idara/Kurugenzi ipi ina Watumishi wengi ukilinganisha na majukumu yaliyopo, Vilevile unasaidia kuwa na mpango wa kurithishana madaraka ‘succession plan’, kuwezesha upandishaji vyeo kwa Watumishi kwa mfumo bora zaidi, kutumia vyema rasilimali watu iliyopo pamoja na masuala mengine muhimu kwa ustawi wa Taasisi.
Mtendaji wa Mahakama ya Rufani (katikati) ambaye pia ni Mgeni rasmi, Sollanus Nyimbi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mafunzo, kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania na kulia ni Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Edith Rwiza.
Picha ya pamoja.

 

 

Comments are closed.