The House of Favourite Newspapers

Watoto chini ya umri wa miaka mitano kupimwa afya

0

1. na Mmoja wa Wadau wa Umoja huo,Kunal Buner jee.
Daktari Mstaafu wa Afya ya Jamii na Familia wa Al Hilal Clinic Street, Dk. Ali Mzige (kushoto) na mmoja wa wadau wa umoja huo, Kunal Buner Jee.
2.Dk. Ali Mzige (kushoto) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
3.Wanahabari wakifuatilia mkutno huo.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

WATOTO walio chini ya umri wa miaka mitano wanatarajiwa kupimwa afya bure Machi 13, 2016 katika kambi maalum iliyoandaliwa na umoja wa jamii ya watu kutoka Bengali nchini India.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Daktari Mstaafu wa Afya ya Jamii na Familia wa Al Hilal Clinic Street, Dk. Ali Mzige ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuendeshwa na Kambi ya Kupima Afya Bila Malipo kwa watoto wa umri huo katika Shule ya Msingi Kibugumo, Kigamboni, Dar.

Alisema umoja huo kwa kushirikiana na Kliniki ya Kimataifa ya Afya ya Uzazi kwa Baba, Mama na Mtoto ya Mikocheni jijini Dar pamoja na Zahanati ya Kiugumo, watatoa huduma za afya ya kinywa na kupima uzito pamoja na ushauri wa lishe kutoka kwa madaktari na matabibu ambapo watakaobainika kuwa na matatizo maalum ya kiafya watapewa rufaa.

(Na Denis Mtima/Gpl.)

Leave A Reply