The House of Favourite Newspapers

Watoto wa Lamar Odom wamlipa fadhila Khloe Kardashian

0

 Staa wa mpira wa kikapu, Lamar Odom.

Las Vegas, Marekani
WATOTO wa staa wa mpira wa kikapu,Lamar Odom, 35, Lamar Jr na Destiny hivi karibuni wamelipa fadhila kwa kumshukuru mama yao wa kufikia,Khloe Kardashian kwa mapenzi ya dhati aliyoyaonesha kwa baba yao tangu alipozidiwa Oktoba 13, mwaka huu.

Akichonga na mtandao maarufu wa burudani nchini Marekani mtu wa karibu kutoka ndani ya familia hiyo alisema watoto hao wamefikia hatua ya kumshukuru Khloe baada ya kuona matumaini ya kupona baba yao.

“Lamar Jr na Destiny wanamshukuru Khloe kwa kuonesha upendo wa dhati kwa baba yao tangu alipokutwa mahututi,wanaamini bila yeye asingefikia hivyo alivyo kwa hiyo wanauthamini sana mchango wake,” kilisema chanzo hicho.Hivi karibuni Lamar alikimbizwa hospitali baada ya kuzidisha matumizi ya dawa za kulevya ambapo alikutwa amepoteza fahamu huko Nevada Brothel.

Leave A Reply